Lord Eyes aikubali hit song ya Darassa ‘Muziki’
Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Bongo, Lord Eyes ameupa tano muziki wa Darassa hasa hit song yake ya wimbo Muziki.Rapper huyo amesema wale wanaofikiri kuwa Darassa amebahatisha katika ngoma hiyo wanakosea kwa sababu Darassa ni msanii mwenye uwezo mkubwa.
Katika hatua nyingine Lord Eyes amewataja baadhi ya wasanii wa Arusha ambao anaona watafika mbali kimuziki. Lord ametaja majina kama Junior Mic kutoka Junior Nakoz, Motra the Future, Rafu Mc, LP, Chaba na Donii kutoka Watengwa.
“Vijana wapo wengi ni nafasi tu hawajapata, unajua muziki si kurap tu au kuimba, muziki una mambo mengi, kuna kuna masuala mengine ya kibiashara zaidi ya kuingia kwenye hii platform ya ushindani,” amesema Lord Eyes.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments: